array(0) { } Radio Maisha | Naibu wa Rais afanya mkutano wa faragha

Naibu wa Rais afanya mkutano wa faragha

Naibu wa Rais afanya mkutano wa faragha

Naibu wa Rais Dkt. William Ruto amefanya mkutano wa faragha na viongozi wa eneo la Magharibi, katika ofisi yake jijini Nairobi huku ajenda kuu ya kikao hicho ikikosa kubainika.

Licha ya kufikirika kuwa mkutano wa kupanga jinsi ya kufanikisha ushindi wa mgombea wa ubunge wa Kibra kwa tiketi ya Jubilee Macdolnald Mariga, ambaye hakuidhinishwa na IEC kufuatia jina lake kukosa katika sajili, aliyekuwa seneta wa Kakamega Bonny Khalwale amesema mkutano huo umelenga kuangazia maendeleo ya Magharibi.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Khalwale vilevile amesema viongozi wa Jamii ya Mulembe wako katika juhudi za kushirikiana ili kufanikisha maendeleo.

Khalwale alikuwa ameandamana na viongozi 6 akiwamo Kiranja wa wengi katika bunge la kitaifa Benjamin Washiali na aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa.