array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa 7 wa wizi wa milioni 72 waachiliwa kwa bondi

Washukiwa 7 wa wizi wa milioni 72 waachiliwa kwa bondi

Washukiwa 7 wa wizi wa milioni 72 waachiliwa kwa bondi

Washukiwa 7 wakiwamo maafisa 3 wa polisi wanaohusishwa na wizi wa shilingi milioni 72, wameachiliwa kwa bondi ya shilingi milioni moja kila mmoja.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Francis Andayi amesema upande wa mashtaka haujawasilisha  ushahidi wa kutosha ili kuendelea kuwazuilia washukiwa hao.

Washukiwa hao Chris Machogu,  Duncan Kaveshi Luvuga, Boniface Mutua, Vincent Owuor, Alex Mutuku na Francis Muriuki wamekana mashtaka dhidi yao walipofikishwa katika Mahakama ya Nairobi.

Baadhi ya washukiwa hao wanatuhumiwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartred na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya G4S kushiriki wizi huo uliotekelezwa tarehe 5 - 9- 2009.