array(0) { } Radio Maisha | Jeshi la Kenya kuendeleza oparesheni ya Somalia, Rais asema

Jeshi la Kenya kuendeleza oparesheni ya Somalia, Rais asema

Jeshi la Kenya kuendeleza oparesheni ya Somalia, Rais asema

Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia ni amiri jeshi mkuu amesema Jeshi la Kenya, KDF litaendeleza oparesheni yake ya AMISON nchini Somalia ili kuwakabili magaidi wa Al- Shabaab.

Akihutubu wakati wa hafla ya kufuzu kwa makurutu 2, 500 katika Chuo cha Mafunzo ya Uanajeshi cha Moi Baracks - Uasin Gishu, Rais amewashauri wanajeshi waliofunzu kudumisha umoja wa taifa huku akitoa hakikisho la serikali kuboresha utendakazi wa jeshi.

Rais amewapongeza wanajeshi wa kike ambao amesema mwaka 2019 wamejitokeza kwa wingi ili kulitumikia taifa hili.