array(0) { } Radio Maisha | Polosi 3 wamakamatwa na pesa bandia Busia
Polosi 3 wamakamatwa na pesa bandia Busia

Maafisa 3 wa polisi akiwamo Afisa Mkuu wa Idara ya Upelelezi kwenye Kaunti Ndogo ya Bungoma Joseph Kahindi wamekamatwa mjini Busia wakiwa na pesa bandia.

Inaarifiwa kwamba Kahindi ambaye ana cheo cha Superintendent, alisafiri kutoka kazini akiwa na maafisa hao wawili kuelekea Busia walikotarajia kutumia fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 4. 3 za noti bandia za dola za Marekani.

Polisi walifahamishwa kuwahusu watatu hao kabla ya kulisimamisha gari walilokuwa wakisafiria na kuwanasa.