array(0) { } Radio Maisha | Papa Francis atuma ujumbe wa heri kwa Wakenya

Papa Francis atuma ujumbe wa heri kwa Wakenya

Papa Francis atuma ujumbe wa heri kwa Wakenya

Rais Uhuru Kenyatta amepokea ujumbe wa heri na baraka kutoka kwa Papa Mtakatifu Francis.

Papa ametuma ujumbe huo kwa Rais na Wakenya kwa jumla alipokuwa akipita katika anga za Kenya kuelekea Roma baada ya ziara ya siku tatu katika mataifa ya Misumbiji, Madagascar na Mauritius.

Katika ujumbe huo uliowasilishwa kwa njia ya radio na kunakiliwa na Idara ya Kuthibiti Safari za Angali, ATC, Papa Francis ambaye pia ni kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, amewatakia Wakenya heri na amani huku akiahidi kuendelea kuliombea taifa hili.

Ikumbukwe kuwa Francis aliwasili jijini Maputo, Msumbiji tarehe 4 mwezi huu kabla ya kuzuru Madagascar na Mauritius.

Mara ya mwisho kwa Papa Francis kuzuru Kenya ilikuwa mwezi Novemba mwaka 2015 wakati wa ziara yake ya kwanza Barani Afrika na hivyo kumfanya kuwa papa wa pili kuzuru Kenya baada ya Papa John Paul II.