array(0) { } Radio Maisha | Chama cha Jubilee kimepata pigo baada ya mgombea wake wa kiti cha ubunge wa Kibra Macdonald Mariga kukosa kuidhinishwa na IEBC

Chama cha Jubilee kimepata pigo baada ya mgombea wake wa kiti cha ubunge wa Kibra Macdonald Mariga kukosa kuidhinishwa na IEBC

Chama cha Jubilee kimepata pigo baada ya mgombea wake wa kiti cha ubunge wa Kibra Macdonald Mariga kukosa kuidhinishwa na IEBC

Chama cha Jubilee kimepata pigo pigo baada ya mgombea wake wa kiti cha ubunge wa Kibra Macdonald Mariga kukosa kuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi IEBC, baada ya jina lake kukosekana katika sajili rasmi ya tume hiyo.

IEBC imesema jina la Mariga halipo katika sajili zake baada ya kupokezwa cheti na chama hicho ili kushiriki uchaguzi mdogo wa tarehe saba mwezi Novemba.

Ni hali ambayo hata hivyo imesababisha majadiliano ya kina baina ya wanachama wa Jubilee na karani wa IEBC aliyejukumiwa kuthibitisha majina ya wagombeaji katika sajili ya IEBC.

Aidha wananchama wa Jubilee wakiongozwa na Bonny Khaluwale wamethibitisha kwamba Mariga alisajiliwa mapema mwaka huu, wakisema wataendelea na mchakato wa kuhakikisha kuwa maelezo yake yanajumuishwa katika sajili hiyo.

Kwa mujibu wa Khaluwale licha ya kuwa Mariga alisajiliwa hivi karibuni ni jukumu la IEBC kuyajumuisha maelezo yake katika sajili yao ili kuhakikisha kila Mkenya anatekeleza jukumu lake kwa mujibu wa katiba.

Amesema watashughulikia suala hilo ndani ya muda wa siku saba walizopewa huku akisisitiza kwamba kampeni zitaendelea jinsi ilivyoratibiwa.

Hata hivyo, Mariga ameeleza kusikitishwa na hatua hiyo akieleza imani kwamba rufaa wanaoyopania kuiwasilisha utatua changamoto hiyo.

Ikumbukwe Chama cha ODM kimemteua Bernad Okoth kuwania nafasi hiyo huku Chama cha Amani National Congress ANC, kilimteua Eliud Owalo kuwa mgombea wake huku Ford Kenya ikimteua Khamisi Butichi.

Kwa jumla, kuna takribani wagombea kumi ambao watamenyama tarehe 7 Novemba ili kumpata atakayerithi nafasi iliyoachwa wazi kufuatia kifo cha Ken Okoth.