array(0) { } Radio Maisha | Waziri wa Mazingira, Keriako Tobiko ameendelea kutetea mpango wa serikali kuwafurusha wanaoishi katika Msitu wa Mau.

Waziri wa Mazingira, Keriako Tobiko ameendelea kutetea mpango wa serikali kuwafurusha wanaoishi katika Msitu wa Mau.

Waziri wa Mazingira, Keriako Tobiko ameendelea kutetea mpango wa serikali kuwafurusha wanaoishi katika Msitu wa Mau.

Waziri wa Mazingira, Keriako Tobiko kwa mara nyingine ametetea mpango wa serikali kuwafurusha wanaoishi katika Msitu wa Mau.

Akiwa mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa ya Mazingira, Tobiko amesema kwamba sharti msitu huo ulindwe ikizingatiwa kwamba ni chanzo cha mito kama vile Mara na Ewaso Nyiro ambayo kwa miaka sasa imekuwa ikiwanufaisha wakazi wa Kaunti za Narok, Kajiado na Mbunga ya Kitaifa ya Wanyamapori ya Maasai Mara.

Tobiko aidha amekana tetesi kwamba kufurushwa kwa wakazi hao kumechochewa kisiasa akisema viongozi wanaoeneza uvumi huo wanalenga kujipatia umaarufu kisiasa.

Ikumbukwe kuwa serikali ina mipango ya kuwahamisha wakazi zaidi ya elfu sitini kutoka msitu huo, mpango ambao umepingwa vikali na baadhi ya wanasiasa kutoka eneo hilo.