×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Mombasa Edgar Kagoni amewachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja

Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Mombasa Edgar Kagoni amewachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja

Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Mombasa Edgar Kagoni amewachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja baada ya kuwasilishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Nairobi Lucas Onyina.

Kuwachiliwa kwake kunajiri siku moja tu baada ya Mahakama Kuu ya Mombasa kuagiza kuwachiliwa kwake kwa bondi ya shilingi laki moja au pesa taslimu shilingi elfu  20 kadhalika kuagiza kutoshtakiwa kwake kwa kuhusishwa na dawa za kulevya aina ya heroin.

Kwa mujibu Hakimu Lucas Onyina, kesi dhidi ya Kagoni itaendelea hadi wakati ambapo stakabadhi halisi zitakapowasilishwa mbele yake.

Hakimu Kagoni alinaswa akihusishwa na kesi ya kupotea kwa dawa za kulevya, zenye thamani ya shilingi milioni 30 aina ya heroin ambazo zlikuwa thibitisho la ushahidi katika kesi ya ulanguzi. Dawa hizo zilipotea baada ya ya kesi hiyo kukamilika na washtkiwa kufungwa miaka 30 gerezani na Kagoni.