array(0) { } Radio Maisha | Aukot afanya mazungumzo na wawakilishi wadi wa Bunge la Bomet

Aukot afanya mazungumzo na wawakilishi wadi wa Bunge la Bomet

Aukot afanya mazungumzo na wawakilishi wadi wa Bunge la Bomet

Kiongozi wa Chama cha Thirdway Alliance, Daktari Ekuru Aukot, amefanya mazungumzo na wawakilishi wadi wa Bunge la Kaunti ya Bomet kuwasihi kuupitisha Mswada wa Punguza Mizigo.

Aukot yuko Bomet kuwarai wawakilishi hao kuunga mkono mswada huo unaolenga kupunguza nafasi za uongozi ili kumpunguzia gharama mwananchi.

Taarifa za awali zinaashiria kwamba huenda Bunge la Kaunti ya Bomet likiwa la kwanza eneo la Kusini mwa Bonde la Ufa kuupitishwa mswada huo.

Licha ya kuwapo kwa pingamizi kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa akiwamo, Kinara wa ODM Raila Odinga kuhusu mswada huo, Aukot ameshikilia kwamba mswada wenyewe utawanufaisha Wakenya pakubwa.

Ikumbukwe Bunge la Uasin Gishu, tayari liliupitisha mswada huo huku Spika wa bunge hilo akitarajiwa kuwasilisha ripoti kwa Spika wa Bunge la Kitaifa, Justin Muturi.