array(0) { } Radio Maisha | Mishra kusisaidia familia mia moja wanaofurushwa kutoka Mau

Mishra kusisaidia familia mia moja wanaofurushwa kutoka Mau

Mishra kusisaidia familia mia moja wanaofurushwa kutoka Mau

Mbunge wa Keses, Swarup Mishra amesisitiza kwamba atazisaidia familia mia moja za watu wanaofurushwa katika Msitu wa Mau.

Akiwahutubia wanahabari kwenye Eneo Bunge lake, Mishra amesema tayari ametenga ekari kumi na mbili za shamba lake kwa manufaa ya familia hizo mia moja.

Mbunge huyo aidha ametoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kuhakikisha watakaofurushwa msituni Mau wanafidiwa kwa kupewa ardhi mbadala.

Amesema ni jambo zuri kutunza mazingira katika msitu huo ila wakazi ambao walitumia fedha zao kununua vipande vya ardhi sharti wafidiwe.

Kauli yake inajiri wakati ambapo baadhi ya wakazi wameapa kwamba hawataondoka katika msitu huo wakisema wana hatimiliki.

Ikumbukwe baadhi ya mawakili wamewasilisha kesi katika Mahakama ya Kitale kupinga ufurushaji wa watu katika Msitu wa Mau wakidai kwamba haki za watoto ambao wanasoma msituni humo zimekiukwa. Mawakili hao wanailaumu serikali kufuatia ilani kwamba shule zote na hospitali eneo hilo zinapaswa kufungwa ili kuruhusu utunzaji wa mazingira.