array(0) { } Radio Maisha | Afisa wa polisi anauguza majeraha baada ya kujeruhiwa na wanafunzi

Afisa wa polisi anauguza majeraha baada ya kujeruhiwa na wanafunzi

Afisa wa polisi anauguza majeraha baada ya kujeruhiwa na wanafunzi

Afisa mmoja wa polisi anaendelea kuuguza majeraha baada ya kujeruhiwa wakati wa makabiliano kati ya maafisa wa usalama na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Multimedia, Kaunti ya Nairobi.

Tayari baadhi ya wanafunzi wametiwa nguvuni huku polisi wakifanikiwa kudhibiti maandamano ya wanafunzi hao yaliyong'oa nanga mwendo wa saa nne leo asubuhi.

 

Polisi wa kukabili ghasia walitumia vitoza-machozi kuwatawanya wanafunzi hao waliokuwa wakiandamana kulalamikia kuuliwa kwa mmoja wao.

Inaarifiwa kwamba mwanafunzi huyo alifariki dunia baada ya kugongwa na matatu ya Chama cha Ushirika cha Ongata Line ililotoweka baadaye. Makabiliano hayo yamesababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye Barabara ya Magadi.