array(0) { } Radio Maisha | ATC:Wanafunzi kutoka Tanzania na Kenya wapata fursa ya kuendelea na Mafunzo Uchina

ATC:Wanafunzi kutoka Tanzania na Kenya wapata fursa ya kuendelea na Mafunzo Uchina

ATC:Wanafunzi kutoka Tanzania na Kenya wapata fursa ya kuendelea na Mafunzo Uchina

Awamu ya 6 ya shindano la Africa Tech Challenge ATC linalopigia debe masomo ya kiufundi imekamilika rasmi huku wanafunzi wa Kenya na Tanzania wakiibuka washindi na kupata fursa na kufanya mafunzo hayo Uchina.

Wanafunzi hao Kimani Githinji Oscar kutoka Chuo cha Kitaifa cha Kiufundi cha Meru na Christopher Tumbembele na Apolo Godwin kutoka cha Kiufundi cha Dar Es Salaam wametaja kufurushwa na fursa hiyo.

Katibu wa Mafunzo ya Kiufundi, TVET katika Wizara ya Elimu Kevit Desai, anasema amefurahishwa na mikakati inayowekwa kuboresha vyuo vya kiufundi na kuishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano wao na kushirikisha mataifa ya Tanzaniana Ethiopia katika mashindano mwaka huu.

Vilevile vyuo vitatu vya Kenya Chuo cha Kenya Technical Trainers Colege, Kiambu Institute of Technology na Kabete National Technology, vilishinda shilingi laki tano kila chuo. Vyuo hivyo vilishinda Tuzo ya Jin Yetao, ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa mafunzo hayo aliyefariki mwezi Machi mwaka huu katika ajali ya ndege ya Ethiopia akiwa na mika 32.

Vilevile katika Tuzo la Makundi, wanafunzi wa Tanzania na wa Chuo cha Kiufundi cha Meru walituzwa shilingi milioni 10.

Mwaka huu mataifa 8 na makundi 16 yalishiriki. Kila taifa liliwasajili wanafunzi watatu na mwalimu mmoja. Mwaka huu mataifa yatakayoshiriki ni Kenya, Tanzania, Uganda, Ghana, Ghana, Gabon, Zambia na Ivory Coast.