array(0) { } Radio Maisha | YATTANI: KRA ihakikishe bidhaa zinazoingizwa nchini ni salama kwa matumizi ya binadamu

YATTANI: KRA ihakikishe bidhaa zinazoingizwa nchini ni salama kwa matumizi ya binadamu

YATTANI: KRA ihakikishe bidhaa zinazoingizwa nchini ni salama kwa matumizi ya binadamu

Wito umetolewa kwa Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi, KRA kushirikiana na idara nyingine serikalini ili kuhakikisha bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia Bandari ya Mombasa ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Kaimu Waziri wa Fedha, Ukur Yattani amesema wafanyabiashara wengi huingiza bidhaa ghushi nchini hali inayotishia ushindani miongoni mwao.

Akizungumza jijini Mombasa, Waziri Yattani aidha amewashauri wakuu wa bandari hiyo kuunga mkono mpango wa serikali kuhakikisha kwamba bidhaa zinazoingizwa bandarini zinasafirishwa kwa reli hadi Nairobi ili kukaguliwa. Amesema ni kupitia njia hiyo tu ndipo shughuli katika Bandari ya Mombasa zitarahisishwa.