array(0) { } Radio Maisha | Kesi ya kutakuwa mzozo wa eneo lililo mpakani pa Kenya na Somalia yahairishwa
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kesi ya kutakuwa mzozo wa eneo lililo mpakani pa Kenya na Somalia yahairishwa

Kesi ya kutakuwa mzozo wa eneo lililo mpakani pa Kenya na Somalia yahairishwa

Kesi kuhusu eneo lililo mpakani pa Kenya na Somalia lenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi imeahirishwa kwa miezi miwili. Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ imeahirisha kusikilizwa kwa kesi hiyo baada ya Kenya kuiomba mahakama hiyo kutoa muda zaidi ili iwateue mawakili wapya watakaoiwakilisha katika kesi hiyo ambayo ilipaswa kusikilizwa wiki ijayo.

Inaarifiwa kwamba Kenya ilikuwa imeomba kesi hiyo kuahirishwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya majaji wa ICJ kuagiza isikilizwe kati ya Novemba tarehe nne na nane.

Hatua hii inajiri wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Bara Afrika ikizitaka Kenya na Somalia kushiriki mazungumzo ya kukwamua utata uliopo kuhusu mipaka katika Bahari Hindi.

Wito huo umetolewa wakati wa kongamano la mia nane sabini na sita la baraza la Umoja huo ambalo limefanyika katika Mji Mkuu wa Ethiopi Adis Ababa. Baraza hilo limetoa wito kwa mataifa haya mawili kujiepusha na mivutano ambayo inaweza kuibua mizozo zaidi.

Wakati wa Kongamano hilo Katibu wa Kudumu wa Kenya katika Umoja wa Afika AU Cathrine Mwangi na Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni wa Somalia, Abdulkadir Ahmed-Kheir wametoa hotuba zao kuhusu uhusiano baiana ya mataifa haya mawili.