array(0) { } Radio Maisha | Kenyatta afungua rasmi Maonesho ya Kilimo jijini Mombasa

Kenyatta afungua rasmi Maonesho ya Kilimo jijini Mombasa

Kenyatta afungua rasmi Maonesho ya Kilimo jijini Mombasa

Rais Uhuru Kenyatta amefungua rasmi Maonesho ya Kilimo ya Mkomani Nyali jijini Mombasa huku akitoa wito wa kuungwa mkono kwa uvumbuzi wa kilimo kutumia teknolojia ya sasa ili kufikia ukuaji wa uchumi kufikia mwaka wa 2030.

Rais Kenyatta amewataka Wakenya kuhudhuria maonesho hayo ili kunufaika na nafasi mbalimbali mbali na kuwataka kukumbatia kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa taifa hili.

Kenyatta aidha amesifia ajenda nne kuu za maendeleo akisema zinalenga kuimarisha uchumi wa Kenya, kubuniwa kwa nafasi za ajira na kwa ujumla kuboresha maisha ya Wakenya

Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na upili eneo la Pwani ni miongoni mwa waliomiminika kwenye Uwanja huo. Ubunifu na Teknolojia katika Kilimo na Biashara ndiyo kaulimbiu ya maonesho haya ya mwaka huu.