array(0) { } Radio Maisha | BBI yalaumiwa kwa kutoalika umma kwa mazungumzo bali iliwatumia maafisa wa serikali kuwaalika maafisa kadhaa

BBI yalaumiwa kwa kutoalika umma kwa mazungumzo bali iliwatumia maafisa wa serikali kuwaalika maafisa kadhaa

BBI yalaumiwa kwa kutoalika umma kwa mazungumzo bali iliwatumia maafisa wa serikali kuwaalika maafisa kadhaa

Imebainika kwamba Jopo la Upatanisho la BBI liliwaalika watu waliofika mbele yake kutoa mapendekezo. Kulingana na Shirikla la Kijamii la Uwazi Consortium, waliowasilisha mapendekezo walielezwa namna na jinsi ya kutoa mapendekezo hayo, hivyo hayatakuwa na manufaa yoyote kwa umma.

Aidha, shirika hilo limesema kwamba kinyume na ilivyotarajiwa, BBI haikualika umma bali iliwatumia maafisa wa serikali kuwaalika maafisa kadhaa. 

Aidha, BBi inashtumiwa kwa kutokuwa na uwazi kwani jopo hilo halina ofisi maalum, nambari ya simu wala mtandao ambapo wananchi wanaweza kuwa huru kuwasiliana nao. Isitoshe, jopo hilo pia halikuweka wazi majukumu ya wanachama wake. 

Amdany vilevile ameeleza kwamba haikuwapo haja ya kubuniwa kwa jopo hilo kwani lilikuwa likiangazia masuala ambayo yamo katika katiba na sheria nyingine ambazo zinahitaji utekelezaji tu. Daisy Amdany ni mmoja wa viogozi wa shirika hilo la Uwazi.

Ikumbukwe Jopokazi hilo lililobuniwa Machi baada ya mapatano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa ODM, Raila Odinga lilikamilisha shughuli ya kukusanya maoni kutoka kwa umma wiki tatu zilizopita na kwa sasa linaandika ripoti ambayo inatarajiwa kuwasilishwa na viongozi hao wawili mwezi uu huu.