array(0) { } Radio Maisha | Wasanii Tiwa Savage na Burna Boy wasitisha tamasha waliopanga kuhudhuria Afrika Kusini kufuatia Xenophobia

Wasanii Tiwa Savage na Burna Boy wasitisha tamasha waliopanga kuhudhuria Afrika Kusini kufuatia Xenophobia

Wasanii Tiwa Savage na Burna Boy wasitisha tamasha waliopanga kuhudhuria Afrika Kusini kufuatia Xenophobia

Ghasia za chuki dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini zinaendelea kukemewa na watu mbalimbali duniani huku taifa hilo likitarajiwa kuathirika kiuchumi.

Tayari wasanii kadhaa wa kimataifa wamesitisha tamasha waliyopanga kuhudhuria nchini humo. Wa hivi punde amekuwa msanii Burna Boy wa miondoko ya Afrobeat nchini Nigeria ambaye ameapa hatawahi kukanyaga Afrika Kusini baada ya ghasia dhidi ya raia wa kigeni kuzuka upya nchini humo.

Kauli yake inajiri saa chache baada ya mwimbaji Tiwa Savage kutangaza kujiondoa kwenye tamasha aliyokuwa amepanga kuifanya nchini humo baadaye mwezi huu kwa sababu ya ghasia hizo. Savage alikuwa amepangiwa kuwatumbuiza mashabiki wake katika jukwaa kuu la tamasha ya DSTV Delicious Jumamosi ya tarehe 21 Septemba mjini Johannesburg.