array(0) { } Radio Maisha | Cherargei: Serikali ibuni jopo litakalo chunguza kufurushwa kwa watu kwenye misitu

Cherargei: Serikali ibuni jopo litakalo chunguza kufurushwa kwa watu kwenye misitu

Cherargei: Serikali ibuni jopo litakalo chunguza kufurushwa kwa watu kwenye misitu

Suala la kufurushwa kwa watu kutoka msituni Mau linaendelea kuibua hisia miongoni mwa viongozi wa kisiasa. Seneta wa Nandi Simon Cherargey ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Haki za Binadamu ameitaka serikali kubuni jopo maalum litakalochunguza visa vya watu kufurushwa kutoka kwenye mistu mbalimbali nchini. 

Akiwahutubia wanahabari muda mfupi uliopita, Cherargey amesema jopo hilo linastahili kuchunguza na kutoa ripoti kuhusu namna wanaoathirika wanaweza kushughulikiwa mbali na kupewa ardhi mbadala.

Aidha Cherargey amesisitiza kuwa suala hilo limeingizwa siasa huku akidai kuwa anachunguzwa na idara za usalama kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya serikali kuhusu mpango wa kuwafurusha watu Mau.

Seneta huyo amesema Waziri wa Mazingira na Bodi ya Uhifadhi wa Mazingira imeagizwa kufika mbele ya kamati yake wiki ijayo, kuelezea mipango waliyoweka kuhakikisha haki za binadamu hazitakiukwa kufuatia mpango huo.