array(0) { } Radio Maisha | Joho kufika mbele ya Kamati ya Uhasibu kwenye bunge la Seneti kuhusu madai ya ubadhirifu wa fedha

Joho kufika mbele ya Kamati ya Uhasibu kwenye bunge la Seneti kuhusu madai ya ubadhirifu wa fedha

Joho kufika mbele ya Kamati ya Uhasibu kwenye bunge la Seneti kuhusu madai ya ubadhirifu wa fedha

Kamati ya Uhasibu kwenye bunge la Seneti CPAIC kesho inatarajiwa kumhoji gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho kuhusu madai ya ubadhirifu wa fedha katika mwaka wa kifedha 2017 / 2018.

Joho atatakiwa kujibu maswali kuhusu deni gushi ineligible bills la bilioni 1.8 ambalo lilinakiliwa kwenye nyaraka za Serikali ya Kaunti hiyo katika mwaka huo, kulingana na ripoti ya Ofisi ya Mkaguzi mkuu wa Fedha za umma iliyotolewa tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu.

Jingine ambalo Joho atakabiliwa nalo ni kuhusu deni la asilimia themanini na sita nukta tatu ambalo serikali hiyo inadaiwa na wanakandarasi mbalimbali vilevile matozo ya kodi ya aslimia kumi na tatu nukta saba yaliyokusanywa mwaka huo.

Kamati hiyo tayari imemhoji gavana wa Kwale Salim Mvurya ambaye alikabiliwa na wakati mgumu wa kuyajibu baadhi ya maswali kuihusu ripoti hiyo ya mwaka 2017 / 2018.

Mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa Moses Kajwang, Mvurya alionekana kulikwepa swali la matozo ya kodi ya Kaunti hiyo baada ya kutakiwa kujibu ni kwa nini katika mwaka huo ni asilimia tatu nukta tano pekee yalitozwa.

Akijibu swali kuhusu nyaraka za mwaka huo wa kifedha zinazoonesha kwamba jumla ya shilingi bilioni moja nukta mbili hazikutumika, Mvurya alisema kwamba hali hiyo ilichangiwa na kucheleweshwa kwa mgao wa fedha kwa Serikali za Ugatuzi  kutoka kwa Serikali ya Kitaifa.