array(0) { } Radio Maisha | Sonko alaumiwa kwa kukosa kuwasilisha kodi ya shilingi bilioni 4.5

Sonko alaumiwa kwa kukosa kuwasilisha kodi ya shilingi bilioni 4.5

Sonko alaumiwa kwa kukosa kuwasilisha kodi ya shilingi bilioni 4.5

Gavana wa Nairobi Mike Sonko ni miongoni mwa magavana ambao wanatarajiwa kufika mbele ya kitengo cha kutatau mizozo ya kodi katika Mamlaka ya Utozaji Kodi.

Sonko analaumiwa kwa kukosa kuwasilisha kodi ya shilingi bilioni 4.5 kutokana na matozo ya mishahara ya wafanyakazi, malipo ya wanakanadarasi na mapato ya kaunti.

Hata hivyo, tayari Sonko ameashiria kuwa huenda asijibu maswali ya KRA kwani suala hilo tayari liko mahakamani.

Amesema atawasilisha agizo la mahakama la kuzuia suala hilo kujadiliwa. Sonko na magavana wengine sita kwa jumla wanadaiwa shilingi bilioni 13. Kaunti ya Kiambu inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 3.2, Kilifi bilioni 2, Migori bilioni 1.3, Murang'a bilioni 1.02, Homa Bay milioni 765 na Turkana milioni 455.