array(0) { } Radio Maisha | Baadhi ya viongozi wa eneo la Bonde la Ufa wazidi kumkashfu Tobiko kwa kuwafurusha watu Mau
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Baadhi ya viongozi wa eneo la Bonde la Ufa wazidi kumkashfu Tobiko kwa kuwafurusha watu Mau

Baadhi ya viongozi wa eneo la Bonde la Ufa wazidi kumkashfu Tobiko kwa kuwafurusha watu Mau

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti Kipchumba Murkomen amesisitiza kuwa hatua ya kuwafurusha watu kutoka Msitu wa Mau, haiungwi mkono na Rais Uhuru Kenyatta huku akishikilia kwamba ni ajenda binafsi ya Waziri wa Mazingira, Keriako Tobiko.

Murkomen amesema Tobiko pamoja na Mshirikishi wa Utawala wa Bonde la Ufa, George Natembeya, wamekuwa wakijifanyia maamuzi bila ufahamu wa Rais Kneyatta hivyo kutumia mamlaka yao visivyo.

Vilevile, Murkomen amesema serikali haijatoa maagizo yoyote ya kuwaruhusu wanafunzi kusoma kwa siku sitini huku akiwasihi wabunge kuwahoji Waziri Tobiko na Natembeya kwa kuendeleza shughuli hiyo bila kuzingatia sheria.

Katika kikao tofauti mbunge wa Cherengany Joshua Kutuny amewashtumu viongozi wa eneo la Bonde la Ufa akiwamo Naibu wa Rais William Ruto, kwa kufeli kuangazia ipasavyo suala la watu kufurushwa kutoka Msitu wa Mau.

Kutuny amesema Ruto na Murkomen wamekuwa wakishirikiana na viongozi wengine wa eneo hilo, kujitafutia umaarufu wa siasa za mwaka wa 2022 badala ya kushughulikia mahangaiko ya waathiriwa.

Hata hivyo Murkomen amepuuza matamshi ya Kutuny.

Majibizano haya yanajiri huku mbunge wa Emurua Dikirr, Johana Ngeno pamoja na wawakilishi wadi wawili wakiachiliwa huru baada ya kuzuiliwa kwa tuhuma za uchochezi kwenye Kaunti ya Narok.

Ng'eno na wawakilishi wadi, Jephason Lang'at wa Ololunga na Samuel Kirui Ilmotyot wameachiliwa bila kufikishwa mahakamani jinsi ilivyotarajiwa, baada ya kufanya kikao cha faragha na mkuu wa upelelezi katika Kaunti ya Narok.

Mbunge wa Chepalungu Gedion Koskei amesema uchunguzi wa wapelelezi umebainisha kuwa watatu hao hawana kesi ya kujibu.

Watatu hao walinaswa jana kwa madai ya kupanga kuwachochea wakazi kupinga hatua ya serikali kuwafurusha kutoka Msitu wa Mau.

Wakati uo huo waliokuwa madiwani wa eneo la Narok wamejitokeza kupinga taarifa kwamba walihusika katika uuzaji wa ardhi za watu wanaofurushwa katika Msitu huo.

Wakiongozwa na Manra Ole Maturi, viongozi hao wa awali wamewashauri waathiriwa kuwashtaki watu waliowauzia sehemu hiyo ya msituni.