array(0) { } Radio Maisha | Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara atakiwa kujiuzulu

Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara atakiwa kujiuzulu

Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Maasai Mara atakiwa kujiuzulu

Mchakato wa kumtaka Naibu Mkuu wa Chuo cha Maasai Mara Profesa Mary Walingo kujiuzulu unaendelea kushika kasi baada ya Viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu , kutoa makataa ya siku saba kwake kuondoka ofisini kwa madai ya ubadhirifu wa shilingi milioni 190.

Kiongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi, Ann Mvurya, ametoa wito kwa Idara ya Upelelezi DCI kuchunguza madai hayo na kumchukulia hatua kali za kisheria profesa huyo.

Kwa upande wake Winne Nyandiga Kiongozi wa Wanafunzi wa Common Weath, ametoa wito kwa serikali kuchunguza matumizi ya fedha katika  taasisi zote za elimu , akisema kwamba wanafunzi wanaendelea kukosa huduma bora huku fedha za maendeleo zikifujwa.

Viongozi hao wameapa kuwashinikiza wenzao kote nchini kwenye maandamano ya kumfurusha Profesa Mary Walingo, iwapo serikali itashindwa kumfungulia mashtaka baada ya wiki moja.

Aidha hapo jana, Chama cha Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu, KUSU vilevile kilimtaka Walingo kujiondoa ili kupisha uchunguzi dhidi yake.

Aidha, chama hicho kinataka manaibu wote wakuu nchini kufanyiwa tathmini ya mali wanayomiliki, ili kubaini iwapo walijipatia kwa njia halali au la.

Haya yanajiri huku Idara ya upelelezi DCI ikiwa tayari ikusanya stakabadhi za kufanikisha uchunguzi wao kuhusu madai hayo.