array(0) { } Radio Maisha | Wakenya 2 waathirika Afrika kusini kufuatia chuki dhidi ya raia wa kigeni

Wakenya 2 waathirika Afrika kusini kufuatia chuki dhidi ya raia wa kigeni

Wakenya 2 waathirika Afrika kusini kufuatia chuki dhidi ya raia wa kigeni

Serikali imesema kwamba inayafuatilia matukio ya chuki dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini xenophobia   baada ya Wakenya wawili kuthibitishwa  kuwa miongoni mwa wanaoendelea kuathirika.

Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni Monica Juma amesema serikali ya Kenya inashirikiana na ile ya Afrika Kusini kuhakikisha Wakenya waliopo nchini humo hawashambuli na makundi ya vijana wanaotekeleza uvamizi huo na kuharibu mali yao

Awali balozi wa Kenya Afrika Kusini, Jean Kamau aliwashariri wakenya walioathirika kufuata maagizo ya polisi na kurekodi ripoti zitakazosaidia katika kuwakabili wahalifu na kuhakikisha wanarejelea maisha yao ya kawaida.

Inaarifiwa watu watano wameuliwa na wengie ishirini na wanane kujeruhiwa wengi wao wakiwa Raia wa Afrika Kusini, tangu uvamizi huo kuanza Jumapili wiki hii.

Hii si mara ya kwanza kwa chuki dhidi ya raia wa kigeni kuripotiwa Afrika Kuisini mwaka 2008 watu sitini na wawili waliuliwa huku watu saba wakiuliwa mwaka 2015 kufuatia visa sawa na hicho.