array(0) { } Radio Maisha | Atakayepeperusha bendera atajulikana Jumamosi; yasema ODM

Atakayepeperusha bendera atajulikana Jumamosi; yasema ODM

Atakayepeperusha bendera atajulikana Jumamosi; yasema ODM
Chama cha ODM kimepuulizilia mbali taarifa kuwa inaenga kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama hicho kuwania kiti cha Eneo Bunge la Kibra kwa njia ya maafikiano. ODM kupitia mtandao wake wa Twitter imezitaja taarifa hizo zilizochapishw akatika gazeti moja la humu nchin kuwa za kupotosha ummaa. Imesemakura ya mchujo itafanyika Jumamosi jinsi ilivyopangwa.
 
Inaarfiwa kuwa hapo kesho Kiongozi wa ODM Raila Odinga anatrajiwa kuongoza mkutano wa viongozi wa chama hicho mojawapo ya ajenda yake ikiwa ni kuafikiana kuhusu atakayepewa tiketi ya chama hicho.
 
Kuna jumla ya wagombea kumi na mmoja wlaioidhinishw ana bodi ya uchaguzi ya ODM kushiriki katika mjucho huo.
 

Kumi na mmoja hao ni Awino Christone Odhiambo, Orero Peter Ochieng’Sine, Tony Ogola Sira, Ojijo Reuben William, Ayako Oguwa, Stephen Okello Okoth, Bernard Otieno Obayi na Obaricks Eric Ochieng.

Wengine ni Owino Brian Shem, Millar John Otieno, Musungu Benson and Owade Lumumba Patrick.

Ikumbukwe vyama vya kisiasa vina hadi Jumapili hii kufanya mchujo na kuwasilisha majina ya wagombea wao kwa Tume ya Uchaguzi IEBC ili kuipa nafasi kwa maandalizi ya uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 7.