array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa, Kilifi

Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa, Kilifi

Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa, Kilifi
Makachero wa Idara ya Upelelezi kwenye Kaunti ya Mombasa wamefanikiwa kuwakamatwa watu wawili mapema leo wakiwa na bangi magunia saba yenye thamani ya shilingi milioni tano.
 
Jared Omondi mwenye umri wa miaka 27 na Caleb Otieno mwenye umri wa miaka 42 wamekamatwa katika eneo la Samburu kwenye Kaunti ya Kilifi wakishukiwa kusisafirisha bangi hiyo kutoka taifa jirani la Tanzania.
 
Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi DCI eneo la Ubarn jijini Mombasa Anthony Murithi amesema kwamba wawili hao walikuwa wakiisafirisha bangi hiyo kwa kutumia gari ambalo ilikuwa na nambari ya usajili bandia.
 
Amesema kwamba nambari halali ya usajili ya gari hiyo aina ya Toyota Ipsun ni KBJ 067 N japo ilikuwa imebandikwa nambari bandia ya usajili KBN 970N.
 
Wawili hao ambao wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Central jijini Mombasa wanadaiwa kulenga kuiuza bangi hiyo kwenye maeneo tofauti ya eneo la Pwani.
 
Wawili hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi uchunguzi dhidi yao utakapokamilika.