array(0) { } Radio Maisha | Waumini wa Kabonokia wahukumiwa kwa kukataa kuhesabiwa

Waumini wa Kabonokia wahukumiwa kwa kukataa kuhesabiwa

Waumini wa Kabonokia wahukumiwa kwa kukataa kuhesabiwa

Mahakama ya Marimanti kwenye kaunti ya Tharaka Nithi imeafunga waumini arubaini na sita wa dhehebu la Kabonokia kati ya miezi sita na mwaka mmoja gerezani kwa kukataa kuhesabiwa wakati wa shughuli ya sensa.

waumini hao walisusia shughuli hiyo wakiitaja kuwa ya kishetani. Jumla ya waumini hamsinio wa dhehebu hilo wa maeneo ya Karocho, Thiiti na Kathangacini wamefikishwa mahakamani leo hii kwa wakikabiliwa na tuhuma za kutatiza shughuli za serikali. Washukiwa wanadaiwa kutokuwa na vitambulisho vya kitaifa mabli na kukataa alama zao za vidolewa kurekodiwa kwenye amshine zilizokuwa zikitumika wakati wa sensa.

Wanne miongoni mwao waliachiliwa baada ya kukiri makosa dhid yao na arubaini na sita kuhukumiwa baada ya kusisitiza mbele ya mahamaa kuwa dini yao haiwaruhusu kushiriki shughuli hiyo.

Uamuzi dhidi yao umetolewa na hakimu  Stephen Nyaga.