array(0) { } Radio Maisha | KRA yaipa idhini Sportpesa kuendeleza shughuli zake

KRA yaipa idhini Sportpesa kuendeleza shughuli zake

KRA yaipa idhini Sportpesa kuendeleza shughuli zake

Ni afueni kwa washiriki wa michezo ya bahati nasibu baada ya Mamlaka ya Ukusanyaji Kodi Nchini, KRA kuipa idhini kampuni ya SportPesa kuendeleza shughuli zake kufuatia kusuluhishwa kwa mvutano kuhusu ulipaji kodi.

Kufuatia hatua hiyo, SportPesa sasa inatarajiwa kutuma upya kwa Bodi ya Kudhubuti Michezo ya bahati Nasibu na Kamati ombi la kupewa leseni ya kuhudumu nchini.

Jana, SportPesa kupitia wavuti wake ilidokeza kwamba ulifanya mashauriano ya kufana na serikali na kwamba ina imani itarejelea shughuli zake hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa serikali iliipokonya SportPesa lesini ya kuhudumu mapema mwezi Julai mwaka huu kwa msingi kwamba ilikuwa miongoni mwa kampuni ambazo zilikuwa zikikwepa kulipa kodi. Kufuatia hatua hiyo, kampuni ilifutilia mbali ufadhili wake nchini yakiwamo matangazo katika vyombo vya habari.