array(0) { } Radio Maisha | ODM yasema uteuzi wa Mackdonald Mariga kuwania ubunge Kibra hauna uzito wowote

ODM yasema uteuzi wa Mackdonald Mariga kuwania ubunge Kibra hauna uzito wowote

ODM yasema uteuzi wa Mackdonald Mariga kuwania ubunge Kibra hauna uzito wowote

Chama cha ODM kimesisitiza kwamba uteuzi wa Mwanasoka Mcdonald Mariga kuwa mgombea wa kiti cha Ubunge katika Eneo la Kibra kwa tiketi ya Chama cha Jubilee hauna uzito wowote.

Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna,  amesema Mariga haungwi mkono na viongozi wote wa Jubilee hivyo hataibuka na ushindi wakati wa kinyang'anyiro hicho cha Novemba 7 mwaka huu.

Amesema ODM itafanya mchujo Jumamosi hii ili kujua ni nani atakayepeperusha bendera yake wakati wa uchaguzi huo mdogo.

Amesema Mariga anatumiwa na Naibu wa Rais, William Ruto kwa lengo la kumenyana na Kinara wa ODM, Raila Odinga.

Kauli yake inajiri saa chache tu baada ya  Mbunge wa Gatundu Kusini,  Moses Kuria kupinga utezi huo, akisema Mariga aachwe ajishughulishe na ukuzaji wa talanta ya soka.

Katika mtandao wake wa twitter, Kuria amemshauri Naibu wa Rais William Ruto kutomwingiza Mariga katika siasa chafu. Hata hivyo akizungumza jana baada ya kuidhinishwa kuwania kiti hicho, Mariga alipinga vikali madai kwamba anatumiwa na Ruto.