array(0) { } Radio Maisha | Mawakili wa Linturi walaumiwa katika kesi ya talaka na Marianne Kitany
×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
×

Mawakili wa Linturi walaumiwa katika kesi ya talaka na Marianne Kitany

Mawakili wa Linturi walaumiwa katika kesi ya talaka na Marianne Kitany

Mawakili wa Seneta wa Meru, Mithika Linturi wamelaumiwa kwa kuibua madai kwamba babaye seneta huyo alifariki kufuatia mshtuko wa moyo baada ya kuambiwa kwamba mkewe Linturi Maryanne Kitany wa jamii ya Kalenjini alimjengea nyumba ilhali ana wanao wenye uwezo wa kufanya hivyo. 

Wakili Danstan Omari amesema inasikitisha kusikia kwamba Linturi kupitia mawakili wake -Muthomi Thiankolu na Profesa George Wajakoyo wanamhusisha babaye Seneta huyo na ushahidi aliotoa Kitany kwamba aligharimia ujenzi wa makazi ya wazazi wa Linturi, vilevile makazi yao eneo la Runda jijini Nairobi.

Wakili Omari amesema vikao hivyo havipaswi kuendelea hasa baada ya mteja wake kuomba kusitishwa kwa muda ili kuruhusu familia ya Linturi kuomboleza.

Hata hivyo, mawakili wa Linturi wakiongozwa na Profesa George Wajakoyo wamesema Kitany analeta mzaha mahakamani kwa kutaka vikao hivyo kusitishwa kwa muda.

Kwa upande wake Wakili Muthomi Thiankolu, vikao hivyo vinapaswa kuendelea kwani si Kitany ndiye amefiwa.

Wakati uo huo, Wakili Omari amesema inashangaza kuona kwamba Linturi anashinikiza vikao hivyo kuendelea wakati ambapo anapaswa kuomboleza kifo cha babaye. Ameiomba mahakama hiyo kuheshimu wafu kwa kusitisha vikao hivyo kwa muda.

Mahakama inasubiriwa kutoa uamuzi wa iwapo vikao hivyo vitasitishwa ili kumpa Seneta Linturi muda kwa kuomboleza kifo cha babaye.