array(0) { } Radio Maisha | Mahakama yatupilia mbali ombi la kutaka kumwondoa Wilson Sossion katika wadhifa wa Katibu Mkuu wa KNUT.

Mahakama yatupilia mbali ombi la kutaka kumwondoa Wilson Sossion katika wadhifa wa Katibu Mkuu wa KNUT.

Mahakama yatupilia mbali ombi la kutaka kumwondoa Wilson Sossion katika wadhifa wa Katibu Mkuu wa KNUT.

Mahakama ya Uajiri na Leba imetupilia mbali ombi la Hesbon Otieno la kutaka kumwondoa Wilson Sossion katika wadhifa wa Katibu Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu, KNUT.

Hesbon ambaye aliteuliwa kushikilia nafasi hiyo kikaimu baada ya Baraza la Kitaifa la KNUT kumwidhinisha, kupitia wakili wake Okong'o Omogeni alilenga kusitisha agizo la kumrejesha Sossion katika wadhifa huo, agizo ambalo lilitolewa na mahakama iyo hiyo.

Kwa mujibu wa Hesbon, kurejeshwa kwa Sossion katika nafasi hiyo kunaibua mkanganyiko katika utendakazi wa KNUT ikizingatiwa uteuzi wake ulipitishwa na Baraza Kuu la chama hicho.

Jaji Hellen Wasilwa amesema Hesbon Otieno na wenzake tayari walikiuka agizo la mahakama lililotolewa na Jaji Byram Ongaya lililoharamisha mkutano uliomg’atua Sossion katika wadhifa huo.

Wasilwa amesema ni jambo la kushangaza kuona Otieno na walimu wenza wakikosa kuheshimu agizo la mahakama ambayo wanaitaka kuwatendea haki.

Wasilwa ameamuru kwamba Sossion aendelee kuhudumu katika nafasi ya Katibu Mkuu wa KNUT hadi kesi hiyo itakaposikilizwa na kukamilika.