array(0) { } Radio Maisha | Mbunge wa Wajir Kaskazini, Ahmed Ibrahim anusurika kifo

Mbunge wa Wajir Kaskazini, Ahmed Ibrahim anusurika kifo

Mbunge wa Wajir Kaskazini, Ahmed Ibrahim anusurika kifo

Mbunge wa Wajir Kaskazini, Ahmed Ibrahim amenusurika kifo baada ya watu wasiojulikana kuuvamia msafara wake na kuliteketeza gari lake kwenye eneo la Masalale. Inaarifiwa kuwa Mbunge huyo alikuwa ameandamana na maafisa ambao walikuwa wanaendenda kuitekeleza shughuli ya sensa.

Inarifiwa uvamizi huo ulitekelezwa punde baada ya maafisa hao kuwasili kwenye eneo hilo linalozonaniwa baina ya Maeneo Bunge ya Wajir Kaskazini na Eldas.

Siku mbili zilizopita, watu wanaoishi mpakani pa maeneo bunge hayo mawili waliandamana wakiitaka serikali kutangaza mpaka rasmi katika eneo hilo. Maandamano hayo yalifuatia tangazo kwamba wenyeji hao walitakiwa kurejea walikozaliwa hadi aple shughuli ya sensa itakapokamilika.