array(0) { } Radio Maisha | Uhuru: Makumbusho ya Jomo Kenyatta ya mwaka huu ndio ya mwisho

Uhuru: Makumbusho ya Jomo Kenyatta ya mwaka huu ndio ya mwisho

Uhuru: Makumbusho ya Jomo Kenyatta ya mwaka huu ndio ya mwisho

Maadhimisho ya makumbusho ya Rais wa kwanza wa Kenya, Hayati Mzee Jomo Kenyatta ya mwaka huu ndio ya mwisho kwa mujibu wa rais Uhuru Kenyatta.

Akizungumza katika Kanisa la Holy Family Basilica, alikoongoza hafla ya 41 ya makumbusho ya tangu kufariki dunia kwa Mzee Jomo Kenyatta, Uhuru amesema kwamba uamuzi huo umeafikiwa baada ya mkutano wa familia yao.

Wakati uo huo amewasuta viongozi ambao wanaendeleza cheche za maneno kuhusu familia za utawala, Dynasties, akisema kwamba uongozi wa taifa haujalishi anakotoka mtu, tabaka lake wala umaarufu ila msukumo wakutaka kuleta mabadiliko na kuwahudumia wananchi.

Uhuru amewataka viongozi wa kisiasa kuweka kipau mbele masuala ya maendeleo badala ya cheche za maneno kuhusu familia hizo.

Wakati uo huo, amewashukuru viongozi watangulizi wa taifa kwa mchango wao akisema kwamba walipigania uongozi wa Kenya kuhakikisha kwamba wananchi wanafurahia ukombozi.

 

Ikumbukwe kuwa Kenyatta aliaga dunia tarehe 22 Agosti mwaka 1978 akiwa kwenye Kaunti ya Mombasa.