array(0) { } Radio Maisha | Kalonzo Musyoka amewasuta Naibu wa Rais, William Ruto na Raila Odinga kwa kuendeleza siasa za mapema.

Kalonzo Musyoka amewasuta Naibu wa Rais, William Ruto na Raila Odinga kwa kuendeleza siasa za mapema.

Kalonzo Musyoka amewasuta Naibu wa Rais, William Ruto na Raila Odinga kwa kuendeleza siasa za mapema.

Kinara wa Chama cha WIPER, Kalonzo Musyoka amewasuta Naibu wa Rais, William Ruto na Kinara wa ODM, Raila Odinga kwa kuendeleza siasa za mapema.

Kwa mujibu wa Kalonzo, wawili hao wamekuwa wakilumbana kila wanapokuwa majukwaani, hali ambayo imeibua joto la kisiasa nchini.

Kauli yake inajiri huku Odinga akikana kutangaza kwamba atawania urais mwaka wa 2022 licha ya kunukuliwa katika mojawapo ya magazeti ya humu nchini.

Aidha, Ruto anasisitiza kwamba yu tayari kumkabili Raila kwenye uchaguzi mkuu ujao, akimkumbusha kukubali matokeo iwapo atashindwa.

 

Wakati uo huo, Kalonzo amewasuta viongozi wanaopora mali ya umma ili kufadhili kampeni za uchaguzi mkuu ujao. Amemsihi Rais Uhuru Kenyatta kutowasaza wanaopora fedha za umma.