array(0) { } Radio Maisha | Mshukiwa wa mauaji ya mjane kwenye Kaunti ya Bungoma asakwa

Mshukiwa wa mauaji ya mjane kwenye Kaunti ya Bungoma asakwa

Mshukiwa wa mauaji ya mjane kwenye Kaunti ya Bungoma asakwa

Maafisa wa Polisi kwenye Kaunti ya Bungoma wanamsaka mwanamume anayeshukiwa kumuua mjane mwenye umri wa miaka 42 ambaye amekuwa wamekuwa wakiishi pamoja.

Mshukiwa mwenye umri wa miaka 46, anadaiwa kumuua Helen Namalwa maarufu  Hadija akimlaumu kuwa uhusiano wa mapenzi na jirani yao.

Hadija ameshambuliwa kwa jembe na kudungwa kisu shingoni huku akifungwa kwa leso kwenye kitanda chao katika kisa ambacho kimewashangaza wakazi wa Kijiji cha Nangeni eneo Bunge la Bumula .

Inaarifiwa mshukiwa yu mafichoni nchini Uganda baada ya kutekeleza kitendo hicho huku akisakwa na polisi. Mwili wa marehemu umehifadhi katika chumba ya maitifa katika Hospitali ya Rufaa ya Bungoma.