array(0) { } Radio Maisha | Washukiwa wa sakata ya NYS wameshtakiwa upya

Washukiwa wa sakata ya NYS wameshtakiwa upya

Washukiwa wa sakata ya NYS wameshtakiwa upya

Washukiwa wa Sakata ya NYS Josephine Kabura, Ben Gethi na wengine wanane wameshtakiwa upya kwenye kesi inayohusisha ulanguzi wa fedha katika Huduma ya Kitaifa ya Vijana NYS.


Upande wa Mashtaka umewasilisha mashtaka mapya dhidi ya Kabura, John Kago Ndungu na Partick Ogola Onyago.
Watatu hao wamedaiwa Desemba mosi 2014 na Mei 30 2015 hapa Nairobi,walihamisha fedha bilioni 90 katika Benki ya K-rep inayomilikiwa na Patrick Ogolla Onyango.


Upande wa Mashtaka umesema kwamba watatu hao walishiriki shughuli hiyo wakijua vyema kwamba fedha hizo ni mali ya wizi kutoka kwa NYS. Mpango huo ulikuwa  kuficha kulikotoka shilingi milioni 791 ambazo pia zimefujwa


Mashahidi 9 kati ya 35 tayari wametoa ushahidi wao katika kesi hiyo. Kesi hiyo itasikizwa mwezi ujao.