array(0) { } Radio Maisha | Wabunge wamependekeza kampuni za kamari zilizopokonywa leseni kuendelea kuhudumu

Wabunge wamependekeza kampuni za kamari zilizopokonywa leseni kuendelea kuhudumu

Wabunge wamependekeza kampuni za kamari zilizopokonywa leseni kuendelea kuhudumu

Serikali imeshauriwa kuruhusu kampuni za bahati na sibu zilizopokonywa leseni kwa tuhuma za kutolipa kodi kuendelea kuhudumu. Wakizungumza na wanahabari jijini Nairobi, baadhi ya maseneta wamesema hatua ya serikali kuzifunga kampuni hizo inatishia kudorora kwa uchumi nchini.

Seneta wa Kakamega, Clephas Malala amesema sekta ya michezo na afya zitaathirika hasa ikizingatiwa kampuni hizo zilikuwa zikitoa ufadhili kwa timu za kandanda nchini vilevile kushirikiana na serikali kuhakikisha mpango wa afya kwa wote, Universal Health Coverage, UHC.

Kauli yake imetiliwa mkazo na Seneta Maalumu, Isaack Mwaura ambaye amesema Kampuni ya SportPesa imekuwa ikiwasambazia vifaa maalumu watu wenye ulemavu wa ngozi, wasio na uwezo wa kuona na wengineo.

 

Mwezi Julai kampuni ishirini na saba zilifungwa kwa madai ya kutolipa kodi.