array(0) { } Radio Maisha | Reuben Ndolo ameachiliwa kwa bondi ya shilingi laki mbili katika kesi

Reuben Ndolo ameachiliwa kwa bondi ya shilingi laki mbili katika kesi

Reuben Ndolo ameachiliwa kwa bondi ya shilingi laki mbili katika kesi

Aliyekuwa Mbunge wa Makadara Reuben Ndolo ameachiliwa huru kwa bondi ya shilingi laki mbili pesa taslimu katika kesi ambapo ametuhumiwa kutumia matamshi ya uchochezi.

Mbele ya Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Milimani Martha Mutuku, Ndolo ameshatakiwa kwa makosa ya kutisha kuua na kusababisha usumbufu. Jana, Ndolo alikosa kufika mahakamani kusomewa mashataka huku wakili wake akidai kwamba alikuwa akiigua.

Mshukiwa alitiwa nguvuni na Makachero wa Flying Squad Jumamosi akiwa na watu wengine sita katika Bustani Gardens katika Barabara ya  Oledume akilaumiwa kwa makosa ya kutisha kuua na kusababisha usumbufu.