array(0) { } Radio Maisha | Profesa Kivutha Kibwana amepuuza uvumi kwamba amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais cha mwaka wa 2022

Profesa Kivutha Kibwana amepuuza uvumi kwamba amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais cha mwaka wa 2022

Profesa Kivutha Kibwana amepuuza uvumi kwamba amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais cha mwaka wa 2022

Gavana wa Makueni Profesa Kivutha Kibwana amepuuzilia mbali uvumi kwamba amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais cha mwaka wa 2022. Kivutha aidha amekana madai ya kuunga mkono azma ya Naibu wa Rais William Ruto akisema atawania kiti hicho.

Kuhusu madai ya kushiriki vikao na Magavana wenzake kutoka eneo la Ukambani  kwa ajili ya manufaa yao, Kivutha vilevile amekanusha madai yenyewe, akisisitiza kwamba mikutano yao imekuwa ya maendeleo. Mapema mwezi huu, gavana huyo alitangaza azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Ikumbukwe maajuzi katika sherehe za Tobong'lore zinazojumuisha jamii za Ateketer katika Kaunti ya Turkana, Kuvutha alisema kwamba Ruto  ni kiongozi ambaye yeyote anastahili kujihusisha naye.