array(0) { } Radio Maisha | Duale kuongoza awamu ya pili ya mazungumzo kuhusu bajeti ya kaunti

Duale kuongoza awamu ya pili ya mazungumzo kuhusu bajeti ya kaunti

Duale kuongoza awamu ya pili ya mazungumzo kuhusu bajeti ya kaunti

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Aden Duale leo anatarajiwa kuongoza wawakilishi wa bunge  katika awamu ya pili ya mazungumzo kutatua utata kuhusu bajeti ya kaunti. Seneta wa Makueni, Mutula Kilonzo Jnr atawaongoza maseneta huku wanachama wengine kwa upande wa bunge wakiwa ni Kiongozi wa Wachache, John Mbadi, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Kimani Ichungwa, Kiranja wa Wachache Junet Mohamed, Amos Kimunya, David Sankok, Makali Mulu na Mishi Mboko.

Wawakilishi wa Seneti ni Prof Margaret Kamar, Johnson Sakaja, Charles Kibiru, Mithika Linturi, Rose Nyamunga, Okong'o Omogeni, Ledma Ole Kina na Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Bajeti Mohamed Mahamud. Kamati hiyo takuwa na muda mwezi mmoja kuanzia leo kumaliza vikao vyake na iwapo wataafikiana kabla ya mbunge yote mawili kurejela vikao rasmi basi watalazimika kuitisha kikao maalum cha bunge.

Bunge limesisitiza kuwa halitalegeza kamba kuhusu msimamo wao wa shilingi bilioni 316.5 licha ya maseneta kusisitiza wanataka shilingi bilioni 335 kiasi cha kuelekea katika Mahakama ya Juu iliyotoa muda zaidi wa mazungumzo.

Tayari Rais Kenyatta ametoa msimamo wake kuhusu suala hilo ambalo huenda likarajea katika Mahakam ya Juu iwapo kamati hiyo maalu  haitaafikiana.