array(0) { } Radio Maisha | Watu wanne wafarikibaada ya kukulachakula katika sherehe za kutoa mahari

Watu wanne wafarikibaada ya kukulachakula katika sherehe za kutoa mahari

Watu wanne wafarikibaada ya kukulachakula katika sherehe za kutoa mahari

Watu wanne wamethibitishwa kufariki dunia katika Kijiji cha Romada, Kieni Magharibi kwenye Kaunti ya Nyeri baada ya kuhudhuria sherehe za kutoa mahari na kula chakula kinachodaiwa kuwa na sumu.

Kwa mujibu wa baadhi ya waliohudhuria sherehe hiyo na familia za waliofariki wameeleza kuwa walianza kuumwa na tumbo baada ya halfa hiyo na baadaye baadhi yao wakaanza kufariki dunia tangu jana.

Mwakilishi wa Wadi ya Mugunda, Mugo Theuri na ambaye ameathirika kutokana na chakula hicho amesema wanakijiji wote walioathirika wamefika katika Hospitali ya Karemeno ili kutibiwa.

Aidha Afisa wa Afya katika Kaunti Peter Wamae amethibitisha kuwa watu saba wamelazwa hospitalini humo na wahudumu wa afya wanachukua vipimo ili kuvipeleka kwenye maabara ili kutambua kilichosababisha hali hiyo.

Wamae aidha amewashauri wanakijiji hao kutokuwa na wasiwasi kwani hali hiyo imedhibitiwa.

Hadi sasa hakuna ripoti kamili kuhusu chanzo cha vifo vya wanne hao.