array(0) { } Radio Maisha | Jamii ya Kuria kuwatuma wawakilishi kwa Kinara wa ODM Ralia Odinga

Jamii ya Kuria kuwatuma wawakilishi kwa Kinara wa ODM Ralia Odinga

Jamii ya Kuria kuwatuma wawakilishi kwa Kinara wa ODM Ralia Odinga

Jamii ya Kuria katika Kaunti ya Migori inapania kuwatuma wawakilishi wao kukutana na Kinara wa Chama cha ODM, Raila Odinga ili kushinikiza kubuniwa kwa Kaunti ya Kuria kupitia Jopo la Upatanishi, BBI.

Viongozi mbalimbali wa jamii hiyo, wakiwamo wa kidini na wa kisiasa wamesema watahakikisha wanakutana na Raila Odinga ili kujadiliana kuhusu suala hilo.

Wakiongozwa na Mbunge wa Kuria Mashariki Marwa Kitayama, viongozi hao wamedai kwamba waliachwa nje katika kura ya maamuzi iliyopita na hivyo eneo la Kuria kukosa kutangazwa kuwa kaunti, wakidai kwamba Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC ilikosa kuidhinisha kufuatia kubuniwa kwake mwaka 1993 badala ya mwaka 1990 jinsi inavyohitajika kisheria.

Kitayama ambaye alichahuliwa kupitia tiketi ya Jubilee aidha amesema angali aanamuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto na kwamba kukutana na Raila Odinga ni moja kati ya mikakati ya kufanikisha azma ya wakazi.

Kwa upande wake Mbunge Maalum wa ODM Dennitah Ghati, amesema mjadala wa kuhakikisha kuwa Kaunti ya Kuria inabuniwa unapaswa kumhusisha yeyote ambaye yu tayari kuwasaidia