array(0) { } Radio Maisha | Wenyeji wa Kaunti ya Taita Taveta walalamikia Uhaba wa maji

Wenyeji wa Kaunti ya Taita Taveta walalamikia Uhaba wa maji

Wenyeji wa Kaunti ya Taita Taveta walalamikia Uhaba wa maji

Kaunti ya Taita Taveta ikiwa mojawapo ya kaunti 11 nchini ambazo zimeorodheshwa na mamlaka ya kukabili ukame, NDMA kuwa ziataathirika na ukame pakubwa, sasa hali hiyo imeanza kujitokeza kwenye kaunti hiyo kufuatia uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo.

Wakazi wa eneo la Bughutta, Marungu na Kasighau wamesema kwa sasa wanalazimika kusafiri kilomita zaidi ya 5 kutafuta rasilmali hiyo ambayo imeadimika, huku wakiwalamu viongozi kwa kutumia changamoto zinazowakumba kujitafutia umaarufu.

Mamlaka hiyo imesema kuwa kaunti za Taita Taveta, Wajir, Garrisa, Narok, Mandera,Turkana, Baringo, Samburu, Pokot Magharibi, Tharaka Nithi, na Tana river ndizo ambazo zitaathirika.