array(0) { } Radio Maisha | Moto wa Githurai 45, ulisababishwa na Mtu

Moto wa Githurai 45, ulisababishwa na Mtu

Moto wa Githurai 45, ulisababishwa na Mtu

Huenda moto uliozuka katika soko la fanicha katika Mtaa wa Githurai 45, Kaunti ya Nairobi ulisababishwa na mtu aliyekuwa na nia ya kuteketeza fanicha hizo zenye thamani ya mamilioni ya pesa.

Uchunguzi wa awali umebainisha kwamba moto huo ulizuka kwenye maeneo tofauti ya soko hilo liliko karibu na Duka Kuu la Kassmart kwenye Barabara Kuu ya Thika.

Wakazi wa eneo hilo wamesema kwamba moto huo ulizuka mwendo wa saa kumi alfajiri na kabla ya kusambaa kwa kasi hadi maduka mengine.

Hakuna aliyejeruhiwa au kuaga dunia wakati wa mkasa huo ambao uliwachukua wazimamoto ziadi ya saa tano kuukabili moto huo.