array(0) { } Radio Maisha | Mfanyabiashara Humphrey Kariuki afikishwa mahakamani

Mfanyabiashara Humphrey Kariuki afikishwa mahakamani

Mfanyabiashara Humphrey Kariuki afikishwa mahakamani

Mfanyabiashara Humphrey Kariuki amefikishwa mbele ya Mahakama ya Milimani na kufunguliwa mashtaka tisa yanayohusu ukwepaji kulipa kodi.

Bilionea huyo alijiwasilisha mahakamani humo wiki mbili baada ya agizo la kumtaka afanye hivyo kutolewa na Idara ya Upelelezi kufuatia agizo la Mkuu wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji.

Kariuki alifika mbele ya Hakimu Francis Andayi pamoja na wafanyabiashara wenza Stuart Geraid na Simon Maundu ambapo walishtakiwa pamoja na kampuni za Africa Spirits Limited na Wow Beverages Limited ambapo wanakabiliwa na mashtaka ya kukwepa kulipa kodi ya jumla ya shilingi bilioni 41 kati ya mwaka 2014 na 2019.

Hakimu huyo alimtaka Kariuki kufika mbele yake tarehe 9 mwezi huu baada ya kukosa kufika mahakamani kabla ya vitengo mbalimbali vya usalama kutakiwa kumsaka baada ya kubainika kwamba alikuwa jijini London.

Hata hivyo, wakili wake Kioko Kilukumi ameiambia mahakama kwamba mteja wake aliyekuwa nje ya nchi na alirejea jana usiku kabla ya kujiwasilisha.