array(0) { } Radio Maisha | Wakazi wa Kibra hawatompigia kura yeyote iwapo si kmazi wa Kibra.

Wakazi wa Kibra hawatompigia kura yeyote iwapo si kmazi wa Kibra.

Wakazi wa Kibra hawatompigia kura yeyote iwapo si kmazi wa Kibra.

Wakazi wa Eneo Bunge la Kibra jijini Nairobi wameapa kwamba kamwe hawatakubali mtu yeyote ambaye si mkaazi wa eneo hilo, kuwania kiti cha ubunge.

Kufikia sasa, jumla ya watu sihirini wamejitokeza na kutangaza kuwa wangependa kuwania  wadhfa huo kwa tiketi ya Chama cha ODM.

Wagombeaji hao elo hii wamefanya mkutano katika uwanja wa Kamukunji kujadili kuhusu mwelekeo wao baada ya taarifa kuibuka kwamba huenda ODM ikampa tiketi ya moja kwa moja atakayepeperusha bendera yake wakati wa uchaguzi mdogo.

Ikumbukwe Baraza Kuu la Chama hicho likitarajiwa kufanya mkutano wake kesho ili kuafikiana kuhusu namna ya kumchagua mgombea wake. Aidha ODM imesema hakitamtangaza atakayewania kiti hicho, hadi pale IEBC itakapotangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mdogo.

Alhamisi wiki hii Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi alikitangaza kuwa wazi kiti hicho hivyo kutoa nafasi kwa IEBC kuandaa uchaguzi mdogo. Kwa mujibu wa sheria tume hiyo inastahili kuandaa uchaguzi huo ndani ya kipindi cha miezi mitatu tangu wadhfa wenyewe kutangazwa kuwa wazi.

Kiti hicho kiliachwa wazi kufuatia kifo cha Ken Okoth aliyefariki dunia kufuatia saratani, Julai tarehe 26, akitibiwa katika Nairobi Hospital.