array(0) { } Radio Maisha | Reuben Ndolo kufikishwa mahakamani Jumatatu

Reuben Ndolo kufikishwa mahakamani Jumatatu

Reuben Ndolo kufikishwa mahakamani Jumatatu

Aliyekuwa Mbunge wa Makadara Reuben Ndolo na washukiwa wengine sita wanaendelea kuzuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani wakisubiri kufikishwa mahakamani Jumatatu.

Saba hao wamekamatwa na maafisa wa Flying Squad kwa madai ya kutatiza amani mtaani Kilimani, Jijini Nairobi. Inadaiwa washukiwa hao wanasemekana walikuwa wakitishia kumuua kwa kumpiga risasi mfanyabiashara mmoja kufuatia mzozo wa ardhi.

Wengine waliokamatwa ni Daniel Otieno Juma,  George Otieno,  Cyrus Nyamboga Gichana , Bernard Ochieng Andai, Dick Otieno Ombaka na   Hassan Dima Wario