array(0) { } Radio Maisha | Odinga akana taarifa kuwa ametangaza kuwania kiti cha urais.

Odinga akana taarifa kuwa ametangaza kuwania kiti cha urais.

Odinga akana taarifa kuwa ametangaza kuwania kiti cha urais.

Raila Odinga amepuuza taarifa zinazodai kwamba ametangaza rasmi kuwa atawania kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Kauli yake inajiri baada ya taarifa hiyo kuchapisha katika gazeti moja nchini ikidai kwamba atakuwa miongoni mwa wale watakaowania kiti hicho na kwamba ndiyo sababu iliyosababisha kupatikana kwa mwafaka baina yake na Rais Uhuru Kenyatta na hata kuahidi kufanyakazi pamoja.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo hii, Odinga ameeleza kusikitishwa na taarifa hiyo akiitaja kuwa propaganda huku asisema kwmaba ni mapema mno kutangaza hatima yake kuhusu uchaguzi mkuu hup.

Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna, Odinga hakulitaja suala la nani atakayewania urais mwaka 2022 wakati wa hotuba yake alipohudhuria hafla ya mazishi ya mama Eva Donde , na kwamba alisisitiza haja ya ushirikiano baina yake na Rais Uhuru Kenyatta.

Sifuna aidha amesema Odinga alizungumzia siasa za mashinani ambazo zinalenga kuimarisha chama hicho na kwamba kamwe hakuzungumzia nani atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Hayo yanajiri huku baadhi ya wanasiasa wa kundi la Kieleweke linalomuunga mkono Odnga pamoja na rais Uhuru Kenyatta likisema kwamba linaunga mkono juhudi za wawili hao kuleta amani nchini. Wakiongozwa na Mbunge Maalum Maina Kamanda, viongozi hao wamesema Raila ana ushawishi mkubwa nchini na kuwataka wanasiasa kutompuuza.