array(0) { } Radio Maisha | wanasiasa wanaomuunga Ruto mkono wasisitiza awaniye kiti cha urais.

wanasiasa wanaomuunga Ruto mkono wasisitiza awaniye kiti cha urais.

wanasiasa wanaomuunga Ruto mkono wasisitiza awaniye kiti cha urais.

Mjadala kuhusu siasa za mwaka 2022, zimeendelea kushika kasi huku wanasiasa wa kundi la Tangatanga linaloomuunga Mkono Naibu wa Rais William Ruto likisisitiza kwamba ametosha kuwania kiti cha urais wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Jumapili hii, Naibu wa Rais William Ruto amewaongoza baadhi ya viongozi katika ziara kwenye kaunti ya Meru. Akizungumza mjini Timau, Ruto amesema kwamba haogopi kamwe, kumenyana na Raila wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, huku akimtaka kukubali kushindwa iwapo Ruto aiabuka mshindi.

Hata hivyo, kwa sasa Ruto amesema hatazingatia siasa kwani lengo lake kuu ni kuwahudumia Wakenya.

Wakati uo huo, baadhi ya viongozi wa Jubilee walioandamana na Ruto aidha wameonya kuwa chama hicho kitakabiliwa na wakati mgumu iwapo akitahakikisha kuwa kimejipanga na kuziweka taratibu zake inavyostahili. Mithika Linthuri ni Seneta wa Meru.

Aidha viongozi hao wameendelea na madai kuwa Raila anatumia ushirikiano wake na rais Uhuru Kenyatta yaani Handshake, kuisambaratisha Jubilee.

Wamesema watazidi kumuunga mkono Rais Uhuru Kenyatta na Ruto ambaye watamuunga mkono mwaka 20200.
Kando na Linturi, viongozi wengine walioandamana na Ruto ni Mbuneg wa Buuri Mugambi Rindiki , Mbuneg Maalum Halima Mucheke , Mbunge wa Njoro Charity Kathambi, Rigathi Gachagua wa Mathira,Mwakilsihi wa Kike a Laikipia Catherine Waruguru na mwenzake wa Naivasha Jayne Kihara .