array(0) { } Radio Maisha | Marafiki wa aliyekuwa Gavana wa Bomet Marehemu Joyce Laboso kuzindua tuzo .

Marafiki wa aliyekuwa Gavana wa Bomet Marehemu Joyce Laboso kuzindua tuzo .

Marafiki wa aliyekuwa Gavana wa Bomet Marehemu Joyce Laboso kuzindua tuzo .

Marafiki wa aliyekuwa Gavana wa Bomet Marehemu Joyce Laboso wamezindua tuzo maalum ili kumuenzi mwendazake.

Tuzo hiyo iliyopewa jina la Dr Joyce Laboso Gneder Award inalenga kusherehekea wanawake na wasichana wenye maono na itatolewa Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.

Tuzo hiyo imezinduliwa katika dhifa iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali serikalini na viongozi wanawake tajika.

Kwa mujibu wa Waziri wa Huduma za Umma, Jinsia na Msuala ya Vijana Magret Kobia, tuzo hiyo inalenga kukumbusha namna Joyce Laboso alivyopigania haki za wanawake nchini.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria hafla ya uzinduzi ya tuzo hilo ni Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi, Beatrice Elachi, Gavana wa Kirinyaga Anne Mumbi Kamotho, Mbunge Maalum Cecily Mabarire, Gavana wa Kitui Charity Ngilu na Katibu katika Wizara ya Vijana na Huduma za Umma Racheal Shebesh.