array(0) { } Radio Maisha | makataa yaliotolewa kwa BBI kukamilika Oktoba 23 mwaka huu.

makataa yaliotolewa kwa BBI kukamilika Oktoba 23 mwaka huu.

makataa yaliotolewa kwa BBI kukamilika Oktoba 23 mwaka huu.

Huku Jopo la Upatanishi, BBI likitarajiwa kuwasilisha ripoti yake kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM, Raila Odinga, jopo la BBI linajumuika katika eneo lisilojulikana kuanzia Jumapili  hii kuandika ripoti , makataa yaliotolewa yakikamilika Oktoba 23 mwaka huu.

Naibu Mwenyekiti Adams Oloo,  amesema maoni ya Wakenya kutoka kaunti zote arubaini na saba yatajumuishwa kabla ripoti hiyo kuwasilishwa kwa wawili hao.

Haya yanajiri huku baadhi ya viongozi wakiishtumu BBI kwa kutochukua maoni katika baadhi ya kaunti nchini. Ijumaa wiki iliyopita Gavana wa Uasin Gishu, Jackson Mandago na mwenzake wa Turkana Josphat Nanok walisema BBI haikuzuru kaunti zao.

Hata hivyo Raila aliwapuuza wawili hao akisema BBI ilizuru kila kaunti kuchukua maoni ya Wakenya. Kwa mujibu wa Raila Wakenya wanapaswa kusubiri mapendekezo ya BBI ili kujua iwapo katiba itafanyiwa marekebisho.

Kwa upande wake Naibu wa Rais, William Ruto anasisitiza kwamba viongozi wanaoendeleza siasa kuhusu suala la katiba kufanyiwa marekebisho wanalenga kuwagawanya Wakenya.